KARIBU DULLAH CAKE KWA BIDHAA BORA

Wednesday, May 11, 2016

WSNGONO ZEMBE CHANZO CHA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

MARTHA MAGAWAZaidi ya asilimia 70% ya wanawake nchini wanamaambukizi ya Virusi aina ya Human Papilo (HPV) vinavyosababisha ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya Kizazi.

Takwimu zinaonesha zaidi ya asilimia 80% ya wanawake wenye ugonjwa huo hufariki ndani ya miaka mitano kwani wengi wao hufika hospitali wakati ugonjwa umeshafika hatua za juu; hayo yamebainishwa na

Dk. Walter Kweka Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Asasi isiyo ya Kiserikali Tanzania Social Outreach Initiative (TASOI) inayojumuisha nguvu za kiweledi, taaluma na uzoefu mbalimbali wa kundi la Watanzania wanaoshirikiana katika kutatua changamoto zinazojitokeza.

Aidha Dk. Kweka ameongeza kuwa tafiti zinaonesha kuwa wanawake wapya wa Kitanzania zaidi ya elfu saba hupata Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa mwaka huku 4,216 kati yao wakifariki dunia.

Tafiti zinaonesha Saratani ya Shingo ya Kizazi huambukizwa kwa njia ya ufanyaji ngono, hivyo wanawake wameshauriwa kuwa na tabia ya kufanya uchunguzi kwa kupima afya zao mara kwa mara kwani kila mwanamke aliyekwisha fanya ngono ana hatari ya kupata ugonjwa huo.

0 comments:

Post a Comment