KARIBU DULLAH CAKE KWA BIDHAA BORA

Friday, May 20, 2016

DIAMOND, ALIKIBA HAWAKAMATIKI

Jana Tasnia ya Muzuki imetoka kushuhudia tukio la kihistoria kwa Hitmaker wa Aje msanii Alikiba akisaini mkataba mkubwa wa kimataifa na kampuni ya Sony Music akiwa msanii wa pili Afrika ukiachana na Davido ambao watakuwa wanasimamia kazi zake kimataifa na kuungana na mastaa wakubwa akiwemo Chris Brown, Beyonce,John Legend na wengine wengi.

Nyota ya Tanzania imezidi kung’aa ambapo Msanii wa Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amepiga bao tena baada ya jina lake kutajwa kwenye mashindano makubwa ya utoaji tuzo za BET akishiriki kama Best International Act in Africa
Artist.

Diamond ameingia kwa mara ya pili katika mashindano hayo ambapo mwaka huu wasanii atakao shindanishwa  ni Wizkid, Yemi Alade, AKA, Black Cofee, Casper Nyovest, Mzvee na Serge Beynaud.

Katika mashindano hayo msanii kutoka Marekani Drake anaongoza kwa jina lake kutajwa katika vipengele tisa akifuatiwa na Beyonce na Rihanna ambapo hao majina yao yapo katika vipengele vitano tofauti.

0 comments:

Post a Comment