Mara baada ya Serikali ya Awamu ya Nne kuahidi ‘Maisha Bora kwa kila Mtanzania’ wananchi walilalama kila kona wakidai kuchoshwa na hali ngumu ya maisha huku wakitaka Rais ajaye awe dikteta ili kuinusuru nchi, kama ambavyo wahenga walivyonena ‘binadamu hana jema’ mara baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani na kuanza kuziba mianya ya rushwa, kukemea ubadhirifu pamoja na kutetea wanyonge tayari wameanza kumwita diktekta.
Maamuzi ya papo kwa hapo yanayofanywa na Rais Magufuli katika operesheni tumbua majipu yamekuwa mwiba kwa baadhi ya vigogo huku wabunge wa upinzani wakijiapiza kuangusha serikali yake kupitia kwa Waziri Mkuu kwa kile walichodai anafumbia macho baadhi ya mambo .
Jambo hili likamuibua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwaonya wale wote wanaomwita Rais ni dikteta na kusema “Wale wanaolalamika Rais ni dikteta wanakosea na wakumbuke Rais ni zao la Awamu ya 3 na ya 4 … kuna vitu ambavyo alijifunza na kimoja wapo alibaini ukitoa majukumu bila msukumo wengi hawafanyi”.
Wakati mambo yakisalia hivyo hapa bara huko Visiwani Zanzibar aliyekuwa Mgombea Urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad, ameibuka katika mkutano wa hadhara Kisiwani Pemba na kusema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein nidikteta na hata maliza kipindi chake cha uongozi hadi 2020.
Kauli hiyo ya Maalim Seif imewaibua vigogo wa CCM visiwani humo na kutaka achukuliwe hatua mara moja kwa kosa la uhaini na kusema “Sivilazimishi vyombo vya dola kufanya ninavyotaka, lakini tunashauri visipuuze ushauri wetu kwa sababu ulimi wa mtu unaweza kuwa sumu hatari kuliko matendo yake,”maneno yake Sukwa Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.
0 comments:
Post a Comment