KARIBU DULLAH CAKE KWA BIDHAA BORA

Sunday, May 22, 2016

JINSI UBUNIFU ULIVYOBADILI RAMANI YA BONGO FLEVA

Mziki wa Bongo Flava umebadilika sana, kutoka kufanya Shoo za bure ili kujitangaza kama walivyokuwa wanafanya wakongwe kama Prof. Jay hadi kufanya matamasha makubwa ya kulipwa kama anavyofanya Diamond Platnumz na timu yake ya Wasafi.Mabadiliko ya teknolojia yamechangia sana ukuaji wa muziki wa Bongo Flava.

Zamani uzalishaji wa mziki huu ulitegemea waandaaji wawili wakongwe Master J na P-Funk Majani pekee, lakini leo hii wasanii wanamiliki Studio zao kama Barnaba na studio yake ya Hightable Sound au Dully Sykes na studio yake ya 4.12.

P FUNK MAJANISoko la mziki limekua sana na hii ni nzuri kwa kiwanda cha mziki Tanzania kwani inahitajika msanii kuwa mbunifu na kujituma zaidi ili kuendelea kuwa bora. Hata kwa waandaaji ‘Producers’ ushindani umeongezeka sana kwani asipotengeneza mdundo mzuri hawezi kupata nafasi ya kufanya kazi na wasanii wakubwa.Kazi sasa imekuwa kwa Promota kuandaa matamasha yenye hadhi ya kisasa ili waweze kutengeneza faida kubwa.

Malipo ya wasanii yamekuwa juu bila kuwa na maandalizi mazuri Promota anaweza kuishia kumlipa msanii kisha yeye akapata hasara. Kizuri zaidi kwasasa wasanii wengi wana uwezo wa kuandaa matamasha au Tour zao wenyewe bila kutegemea Promota.Haya ndio mabadiliko ya kweli kwenye Kiwanda cha Mziki Bongo ‘Bongo Flava’.

0 comments:

Post a Comment