KARIBU DULLAH CAKE KWA BIDHAA BORA

Sunday, May 22, 2016

ADHABU UTAKAYOPATA UKIVUTA SIGARA HADHARANI UGANDA

Sheria mpya na kali dhidi ya uuzaji na uvutaji sigara Uganda yaanza kutekelezwa.

Wavutaji sigara watahukumiwa kifungo cha miezi miwili gerezani au kutozwa faini ya dola 60 iwapo watapatikana wakivuta sigara maeneo kama migahawa,baa na sehemu zingine za umma.

Aidha sheria hiyo mpya pia itawaruhusu wavutaji sigara kuwa umbali wa mita 50 kutoka maeneo ya umaa kama shule,hospitali na maegesho ya teksi wakiwa wanavuta sigara.

Vile vile sheria hiyo imepiga marufuku uuzaji wa sigara za elektroniki al maarufu ‘Shisha’ ambayo imekuwa maarufu katika kila klabu mjini Kampala.

Serikali itachukua hatua kali dhidi ya wauzaji wa sigara moja moja na pia kuweka vikwazo dhidi ya matangazo ya bidhaa za sigara .

Watu chini ya miaka 21 hawatoruhusiwa kununua sigara.

Uvutaji wa sigara si jambo la kawaida nchini Uganda ingawaje mamlaka imeingiwa na wasiwasi kwa kuwa na ongezeko la matatizo ya afya yanayosababishwa na sigara kama vile Saratani,magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu.

0 comments:

Post a Comment