Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ameiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwaondoa wafanyabiashara wanaouza nyama kiholela nje ya machinjio ya Vingunguti.
Pia, amezitaka halmashauri zote tatu za Kinondoni, Ilala na Temeke kujenga machinjio ya kisasa yatakayofanya nyama kupata soko ndani na nje ya nchi kwa kuchinja ng’ombe 1,500 badala ya 500 kwa siku ili kukuza uchumi wa nchi.
Makonda aliyasema hayo alipokwenda kuzindua machinjio hayo baada ya kufungiwa kwa takiribani miezi miwili na Mamlaka ya Dawa na Chakula Tanzania (TFDA) kutokana na mazingira kuwa machafu.
Alisema wafanyabiashara ambao wanauza nyama nje ya machinjio hayo kwa mafungu ni kuhatarisha afya za walaji kwa kuwa nyama zinazouzwa maeneo hayo mara nyingi zinakuwa hazijapimwa.
0 comments:
Post a Comment