KARIBU DULLAH CAKE KWA BIDHAA BORA

Thursday, May 12, 2016

LIPUMBA – DR. MAGUFULI ANANYANYASA WAFANYABIASHARA

Rais Dk. Magufuli alipiga marufuku uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi bila ya kuwa na kibali cha serikali mapema mwaka huu ili kuondoa ushindani usio rafiki kwa viwanda vya ndani vya bidhaa hiyo, Prof. Ibrahim Lipumba, Mtaalam aliyebobea kwenye masuala ya Uchumi,amenukuliwa hivi karibuni akisema Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli anatumia cheo kuwanyanyasa wafanyabiashara.

Lipumba ameyasema hayo katika mahojiano ya moja kwa moja na Kituo kimoja cha Runinga hapa nchini wakati akichambua sakata la ufichwaji wa sukari nchini.Amesema kuwa endapo angekua anakaa na Rais Magufuli angehakikisha kunakuwepo na utaratibu wa uagizaji wa sukari kwa watu ambao ni waaminifu ambao hawatakwepa kodi zilizowekwa na kuagiza sukari ili pamoja na gharama na faida iweze kuuzwa kwa bei ya Tsh 1,800 ili viwanda vya ndani vinavyozalisha sukari viweze kulindwa.

“Tuepukane na kufanya mambo mazito ya sera kwenye majukwaa ya siasa na kuwatisha wafanyabiashara katika hali ambayo haiendani na hali halisi iliyopo”amesema

Prof. Lipumba.Hayo yanakuja siku chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kutangaza kutaifisha tani za sukari zitakazokamatwa zikiwa zimefichwa na wafanyabishara kwenye maghala na kisha kuzigawa kwa wananchi bure.

Hata hivyo imeripotiwa  hivi karibuni kuwepo kwa malalamiko ya kupanda bei ya sukari kutoka kikomo cha bei elekezi ya shilingi 1800 kwa kilo hadi kati ya 2,500 na 2,800.

Jiunge nasi 

0 comments:

Post a Comment