KARIBU DULLAH CAKE KWA BIDHAA BORA

Tuesday, May 10, 2016

MAGUFULI AWARUKA FUTI 100 MATAJIRI

Baada ya wananchi kushuhudia sarakasi zilizokuwa zikipigwa na watia nia wa urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka jana na hatimaye kubaki na tano bora iliyopitishwa na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CC) na Mkutano Mkuu; hatimaye jina la Mgombea Urais aliyepeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu Dk. John Pombe Magufuli lilipatikana.

Vita ya kuzisaka kura za wananchi katika uchaguzi huo ikatawaliwa na mbwembwe za kila namna katika kampeni kati ya aliyekuwa Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) chini ya mwavuli wa Ukawa, Edward Lowassa na aliyekuwa Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Magufuli na kupelekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)  kumtangaza Dk. Magufuli kuwa mshindi Oktoba 29 na kuapishwa Novemba 5 mwaka jana kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hivi karibuni Rais Magufuli amenukuliwa na Vyombo mbalimbali vya Habari akisema serikali yake itaendelea kutetea na kusimamia haki za wanyonge kwani anaamini wao ndio waliomchagua kwa kura nyingi kuliko matajiri katika kinyang’anyiro cha urais Oktoba mwaka jana katika Uchaguzi Mkuu.

0 comments:

Post a Comment