Kutongoza sio kazi rahisi kama unavyodhani inahitaji kujiamini na kujipanga kwa maneno matamu, ila tambua kuna mawili; kukubaliwa au kukataliwa, hivyo ni vyema ukawa makini ili lengo litimie kwa kuzingatia yafuatayo hasa pale unapomtongoza rafiki yako wa karibu.1. Kuwa mwanaume bora
Katika dunia tunayoiishi kila mwanaume anatamani kuwa na mwanamke bora zaidi, hivyo kutaka kuwa na mwanamke unayempenda lazima uwe bora kuliko wengine, hii ni kuanzia tabia zako, vile unavyohusiana
na wengine, miondoko yako, unadhifu wako kuwa mwanaume bora hakuna njia ya mkato, lazima ufuate mkondo ambao wengi hawaufahamu.
2. Msifie
Leo amekuwa tofauti kimuonekano? ama leo amebadilisha hairstyle yake? kama umependezwa na mwanamke mara nyingi utakuwa unavutiwa na
mabadiliko yeyote ambayo ameyafanya hivyo chukua nafasi yako kumsifia vile inavyotakiwa.
Kutumia maneno kama “ngozi yako laini, hivi wakati wote unakuwa hivi?” au “nimependa shati lako na vile jinsi limekubana katika mwili wako” hakufai. Kusifu kwa aina hii usithubutu kutumia kwa sasa kwani
unaweza kuharibu mpango mzima.
3. Tafuta muda wa Falagha
Kumsuka mwanamke huwa ni bora zaidi wakati ambapo mko nyinyi wawili peke yenu, kumsuka mwanamke mbele ya marafiki zako kutamfanya kukuona wewe hautilii mkazo na mambo unayotamka hivyo ni bora wakati ambapo unachukua muda na kuwa na yeye peke yenu mnaongea, unaweza kumsuka kwa kutumia mizaha wakati ambapo mko na marafiki zenu.
Lakini wakati ambapo mko nyinyi wawili, tumia maneno ambayo hatayasahau kiurahisi. Mfano unaweza kumwambia“umenifanya nifurahie siku yangu”, “kukaa na wewe hapa najiskia niko huru”.
Ujanja hapa ni kutumia maneno ambayo yatamfanya yeye kujiona spesho kuliko yeyote na amini usiamini mwanamke kama huyu atakuwa akifikiria mazungumzo yenu kwa muda mrefu.
4. Wanawake wanapenda ucheshi
Hivi wewe ni mcheshi? kama jibu lako hapana basi usiendelee kusoma zaidi ya hapa mpaka uifahamu sanaa ya ucheshi, nadhani unafahamu ya kuwa njia ya kumvutia mwanamke lazima utumie lugha ya ucheshi mara kwa mara, uzuri ni kuwa si lazima uwe na ustadi
wa kuchekesha, unaweza kuelezea matukio yako ya awali ambayo uliona yalikuchekesha, kama mwanamke anaonyesha dalili za kukupenda, basi kila neno utakalolitoa kiutani atacheka.
5. Msumbue mara kwa mara
Wakati mwingine kumsuka mwanamke kunaweza kuonekana kuwa ni kazi ngumu, lakini kitu muhimu ni yale mambo madogo madogo ambayo mnafanya.
Kumsuka mwanamke si kutumia maneno matamu ya kimapenzi pekee bali pia zile tabia ambazo mnafanya wakati mnapokuwa mnaongea. Hii ni kuanzia kucheka hadi migusano yenu ya mara kwa mara.
Kama wote wawili mnakuwa na furaha wakati mnapoongea, hiyo tayari ni njia moja rahisi ya kuashiria unamsuka. Kwa hiyo kuivuka mipaka ya urafiki, unafaa kuivuta miguu yake mara kwa mara upande wako wakati ambapo ameongea kitu cha kuchekesha ama mnapocheka.jiunge nasi
0 comments:
Post a Comment