Kwenye miaka ya 2000 staili ya kuchana ilishika hatamu ambapo msanii kama TID, Mangwea, Profesa J, Juma Nature, Fid Q, Afande Sele na wengine kibao walitikisa game ya muziki wa Bongo Fleva huku kila mmoja akiwa na staili yake inayomtambulisha na kufanya wajulikane na kupata umaarufu.
Hivi sasa game ya Bongo Fleva dizaini kama ladha unapotea siku hadi siku kutokana na kuwepo kwa baadhi ya wasanii kuigana sauti kama ambavyo imekuwa ikidaiwa na baadhi ya mashabiki wa muziki huo, Hit Maker wa wimbo wa Aiyola kuwa moja kati ya wasanii wanaomuiga sauti Star wa Bongo ambaye pia ni meneja wake DIAMOND PLATNUMZ kupitia 255 ya XXL Harmonize amesema“Ukizungumzia Diamond unazungumzia mtu ambae anamelody ya malalamiko ambayo zimeganda kwenye vichwa vya watu wengi kwa hiyo ukiimba malalamiko lazima utafananishwa,
lakini huu ni wakati mzuri wa kutambua huyu ni Harmonise huyu ni Diamond”Baada ya kufanya kolabo ya ngoma yaBado iliyobamba na kumuweka Harmonize katika nafasi nzuri kimuziki hivi karibuni amezawadiwa gari aina ya Mark X kutoka kwa uongozi wa WCB, bonyeza hapa chini kumsikiliza akifunguka zaidi
0 comments:
Post a Comment