Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda wamegundua Sukari iliyofichwa katika jengo la ghorofa tisa ambalo liko katika jengo linalojengwa katika eneo la Hananasifu -Kinondoni huku mmiliki wa sukari hiyo
Bw,Bashir Ismail mwenye asili ya kiasia akitiwa mbaroni na jeshi la Polisi.Sukari hilo inadaiwa kuingizwa usiku katika jengo hilo huku kikiwa katika mifuko ya viroba vya kilo 25,na ishiri lakini pia ikifungwa katika mifuko midogo ya Plastiki ya kilo moja moja.
Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari amesema baadhi ya wafanyabiashara wameendelea kukaidi agizo la serikali kwa kuficha sukari katika maghara na maeneo mbali mbali na kuahidi kuwa Oparesheni dhidi ya wafanyabiashara hao ni ya kudumu.
Bw, Bashir Ismail ambaye alikuwa chini ya Ulinzi wa jeshi la Polisi alihojiwa na kudai sukari hiyo iliyohifadhiwa katika jengo hilo inapelekwa katika vituo vya kijamii ingawa alishindwa kujieleza jinsi mazingira iliyowekwa huku ikifanyika kazi ya kuweka katika viroba kwa kuwa eneo hilo linafanyika ujenzi na sio kiwandani.
0 comments:
Post a Comment