KARIBU DULLAH CAKE KWA BIDHAA BORA

Monday, May 23, 2016

WABUNGE WAPIMWE NA ‘ALCO – BLOW’ KAMA MADEREVA WALEVI

Miaka ya hivi karibuni Mashirika na Taasisi mbalimbali ikiwemo Sumatra na Kampuni ya Bia Serengeti (SBL) yalikabidhi kwa Jeshi la Polisi vifaa maalum vya kupima ulevi kwa madereva wanaoendesha vyombo vya usafiri wakiwa wamelewa.

Tangu kuanza kwa zoezi hilo mafanikio yameonekana kwani idadi ya madereva walevi imepungua kwa kiasi kikubwa na kuepusha ajali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara;

sasa tuachane na upande wa barabarani turudi katika mhimili wa Bunge ambao kimsingi ndio hutunga sheria na kuisimamia serikali.

Mwishoni mwa wiki Bunge lilipakwa matope baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kuingia bungeni na kujibu maswali yaliyoelekezwa katika wizara yake akiwa amelewa! hii ni aibu tena fedheha kwelikweli kwa bunge na taifa kwa ujumla!

Lakini kubwa na la kuudhi zaidi kwa viongozi hawa walioaminiwa na kupewa dhamana na wananchi ni hili aliloibua Spika wa Bunge Job Ndugai kwamba si Kitwanga pekee wapo wabunge ambao huingia bungeni wakiwa wametumia vilevi vikali kama vile bangi, viroba na dawa za kulevya. 

Ndugai akasema“Maana sio ulevi tu, kuna sigara kubwa (bangi), unga (dawa za kulevya)… watu wanapiga konyagi hadi mchana, kimsingi mambo ni mengi, tatizo ni kubwa kiasi”.

Kwa masikitiko makubwa mtembezi.com inahoji, kwa hapa Bunge lilipofikia taifa linakwenda wapi? Kwanini mashirika na taasisi  zilizolisaidia Jeshi la Polisi  kutoa vifaa maalum wa kupima madereva walevi yasiligeukie Bunge hivi sasa na kutoa vifaa hivyo ili kuwabaini wabunge walevi ambao wanachafua sura ya taifa?

0 comments:

Post a Comment