KARIBU DULLAH CAKE KWA BIDHAA BORA

Monday, May 23, 2016

WEMA SEPETU AVUNJA REKODI TZ KAMA RINGOOOO

Tafiti za hivi karibuni zinaonesha zaidi ya nusu ya matajiri wajasiriamali duniani ni Wachina ambapo wataalamu wanasema hii inatoka na muasisi wa nchi hiyo Mao kutamka kuwa wanawake wanamiliki nusu ya mbingu hivyo kuanzia hapo ndio ulikuwa mwanzo wa wanawake wachina kuamka na kuanza kujituma.

Matajiri wakubwa wanawake wanaotokea china ni Zhang Yin, Wu Yajun na Chen Lihua; wengine ambao sio Wachina ni Oprah Winfrey ambaye anaaminika kumiliki utajiri mkubwa kutokana na jitihada anazozifanya.

Hali kadhalika kwa upande wa Tanzania kumekuwa na mwamko kwa wanawake wanaojitambua kuamua kufanya ujasiriamali kwa kubuni biashara binafsi ambazo huwaingizia kipato mfano Mwanamitindo wa kimataifa kutoka Tanzania Flaviana Matata aliyezindua hivi karibuni rangi za kucha ikiwa ni moja ya mbinu za kujikwamua.

Sasa baada ya mlimbwende Wema Sepetu kuzindua ‘lipstick’ ya Kiss, mapema jana aliamua kuongeza wigo wa biashara kwa kuzindua ‘app’ yake ambayo itakuwa inahusisha stories zake binafsi, zenye ukweli na uhakika na mashabiki zake wataweza kupata video clips, audio na picture zinazomhusu mrembo huyo.

Wema amevunja rekodi kuwa mwanamke wa kwanza Tanzania na Afrika kumiliki ‘Mobile App’, kama ambavyo Kapteni Hilda Wendy Ringo alivyovunja rekodi kuwa mwanake wa kwanza kurusha ndege Tanzania.

 Mobile Application ya Wema sepetu itapatikana kwa watumiaji wa ‘smart phone’ simu za kawaida.

0 comments:

Post a Comment