KARIBU DULLAH CAKE KWA BIDHAA BORA

Friday, May 20, 2016

CUF: WAZIRI MKUU ANASTAHILI KUWAOMBA RADHI WATANZANIA

“Moja ya Tatizo Kubwa Tulilonalo Watanzania Hatutaki Kazi” Hii ni kauli ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hivi karibuni alipokuwa mjini London nchini Uingereza baada ya kuulizwa kwanini serikali ya awamu ya tano wamezuia kurusha Bunge Live.

Ambapo alifafanua zaidi na kueleza kuwa kusitishwa kwa bunge kuoneshwa live ni kutokana na kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu ya Rais Magufuli inayowataka watu wafanye kazi ndio maana bunge halionyeshwi live ili watu wafanye kazi kwa maendeleo ya Taifa.

Kauli hiyo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa imetokea kupingwa na wadau mbalimbali, ambapo leo Chama cha Wananchi CUF kupitia Mwenyekiti wa kamati ya Uongozi Twaha Taslima kimelaani kitendo hicho cha walinzi mkuu na kumtaka awaombe radhi watanzania kwa kuwadhalilisha kwa kusema hawataki kazi.

Na kuongeza kuwa kauli hiyo ni kutaka kuwarudisha watanzania kwenye uwoga na kutoiwajibisha serikali eti kwa kisingizio cha Hapa Kazi Tu jambo ambalo linaiua Demokrasia.

0 comments:

Post a Comment