Watanzania kama wangeweza kuwa kitu kimoja na kuvaa utaifa kisha kutoa nguvu kwa kila anayewakilisha taifa huenda mambo yangekuwa tofauti na leo.
Mfano mzuri ni kwenye Tasnia ya Burudani Alikiba ametoa Aje, mashabiki zake wanamweleza jinsi wanavyoweza lakini pia upande wa Chibu akitoa ngoma pia hivyo hivyo, hii sinema pia ipo kwa Yanga na Simba.
Msimu huu Yanga wamefanya vizuri baada ya kutolewa Ligi ya Mabingwa wakadondokea CAF ambako wameingia hatua ya robo fainali.
Pia Yanga itacheza michuano ya Klabu Bingwa ambayo mwakani itakuwa na sura tofauti na Yanga itaingia tena kwa kuwa imechukua ubingwa, wakati Azam itashiriki Kombe la Shirikisho.
Yanga bado haijakata kiu ya mashabiki wake kwani inatakiwa ishinde hatua ya makundi ili iingie nusu fainali ivune pesa nyingine.
Hawa ndiyo wababe 8 walioingia Robo fainali ya michuano ya shirikisho.
1.MoBejaria (Algeria)
2.TpMazembe (DRC)
3.Madeama (Ghana)
4.Al-Ahli Tripoli (Libya)
5.Fus Rabat (Moroco)
6.Kawkab Marrekech (Moroco)
7.Etoile Du Sahel (Tunisia)
8.Young Africans (Tanzania)
Hatua ya makundi itapangwa Mei 24,2016 na timu zitakuwa nne timu mbili za juu kwa kila kundi zitaingia Nusu Fainali.
0 comments:
Post a Comment