KARIBU DULLAH CAKE KWA BIDHAA BORA

Friday, May 20, 2016

YANGA KUWASILI KIBABE

Mashujaa wa Taifa, Yanga SC wanatarajiwa kurejea Dar es Salaam kesho mchana wakitokea Angola, ambako jana walikata tiketi ya kuingia hatua makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika.

Yanga juzi ilifungwa bao 1-0 na wenyeji Sagrada Esperanca katika mchezo wa marudiano wa mchujo wa kuwania hatua hiyo Uwanja wa Esperanca mjini Dundo, Angola.

Yanga wanakwenda hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 2-1, baada ya awali kushinda 2-0 Dar es Salaam, mabao ya Simon Msuva na Matheo Anthony.

Matokeo hayo si tu yana maanisha Yanga inatinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho kwa mara ya kwanza katika historia yake, bali pia inakuwa timu ya kwanza ya Tanzania kufika hatua hiyo ya michuano hiyo.

0 comments:

Post a Comment